Takriban Wairani milioni 3.2 wametoroka makazi yao na kukimbilia katika maeneo salama ndani ya Iran tangu kuanza kwa vita kati ya nchi hiyo na Israel na Marekani, Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) limetangaza leo Alhamisi, Machi 12.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Kati ya kaya 600,000 na milioni 1 za Wairani kwa sasa wametoroka makazi yao na kukimbilia kwa muda katika maeneo salama ndani ya nchi kutokana na mzozo unaoendelea, ikiwa nisawa na watu milioni 3.2,” UNHCR imesema katika taarifa, ikiongeza kuwa “idadi hii inatarajiwa kuendelea kuongezeka mradi tu uhasama unaendelea.”

Milipuko kadhaa yatikisa Tehran

Wakati huo huo mfululizo wa milipuko mikubwa iliitikisa katika mji mkuu wa Iran, Tehran, siku ya Alhamisi, Machi 12, kulingana na mwandishi wa habari wa AFP, siku ya kumi na tatu ya mapiano kati ya Iran, Israel, na Marekani.

Moshi umeongezeka kutoka magharibi mwa mji mkuu, lakini haikuwezekana katika hatua hii kubaini maeneo yaliyolengwa na mashambulizi yanayoendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *