
Kamanda Mkuu Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema vijana wa ardhi hii takatifu watalinda heshima ya Iran kwa nguvu na azma hadi tone la mwisho la damu
Meja Jenerali Amir Hatami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amebainisha kwamba wana wa taifa hili wataendelea kulinda na kutetea ngome za heshima na utu wa Kiislamu wa Iran kwa ujasiri, nguvu na kujitolea kamili.
Jenerali Hatami, katika ujumbe siku ya Jumatano, ikiwa ni kwa heshima ya mazishi ya makamanda waliouawa shahidi katika Vita Vya Kulazimishwa vya Mwezi wa Ramadhani ameandika:
“Katika nyakati za ushujaa na kujitolea, uwepo wa wapiganaji wenzetu na wanajihadi huutia moyo nguvu. Kupaa kwao ni tukio la kuhimidiwa, na hakika wamepata bahati ya kufikia neema na daraja ya juu ya Uislamu, yaani kuuawa shahidi, kushika hadi katika Ridhwan, daraja ya juu kabisa ya Pepo.”
Amesisitiza kwamba watoto wa waaminifu wa Imam Khomeini na Ayatullah Khamenei (rahma za Mungu ziwe juu yao), kama Malik al-Ashtar, wataendelea kutetea na kuhifadhi ardhi yao hadi tone la mwisho la damu.
Hafla ya mazishi ya makamanda hao waliouawa katika mashambulizi ya kigaidi yaliyotekelezwa na Marekani na utawala wa Kizayuni, imefanyika jana kutoka mbele ya Chuo Kikuu cha Tehran kuelekea kituo cha Me’raj al-Shohada, kituo maalumu cha maziko ya mashahidi kilicho kusini mwa Tehran.