Korea Kaskazini imepongeza Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei kwa kuchaguliwa kwake kuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Korea Kaskazini imempongeza Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei kwa kuchaguliwa kwake kuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Shirika la Habari la Serikali ya Korea Kaskazini limetangaza kuwa Pyongyang inaunga mkono rasmi uchaguzi wa Ayatullah Seyyed Mojtaba Khamenei kuwa kiongozi muadhamu wa Iran, na inakemea vikali uvamizi wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya taifa hili la Kiislamu.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini pia imetoa tamko kukemea hatua za kikatili za Marekani na utawala wa Kizayuni, pamoja na mashambulizi “yasiyo halali” dhidi ya Iran. Korea Kaskazini imesema uchokozi huo dhidi ya Iran unavuruga amani na kuongeza hali ya kutokuwa na utulivu duniani.

Korea Kaskazini imetangaza kuwa, kutokana na mgogoro katika eneo la Asia ya Magharibi unaosababishwa na vitendo vya kichokozi vya Marekani, imefanya jaribio la kombora la kimkakati la cruise lililoundwa kwa ajili ya kuzamisha meli kivita.

Kwingineko,, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov, katika mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyyed Abbas Araghchi siku ya Jumanne, amesisitiza kukemea uvamizi wa kijeshi unaotekelezwa na Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran. Aidha amewasilisha pongezi rasmi kwa kuchaguliwa kwa Ayatullah Seyyed Mojtaba Khamenei kuwa Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mnamo Machi 8, 2026, Ayatullah Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei alichaguliwa kuwa kiongozi wa tatu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa kura za Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Muadhamu nchini Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *