
Wizara ya Ulinzi ya Saudi Arabia imetangaza leo Alhamisi, Machi 12, kwamba imedungua ndege isiyo na rubani ya Iran iliyokuwa ikijaribu kukaribia eneo kunakopatikana balozi mbalimbali huko Riyadh. Katika siku ya 13 ya vita, mashambulizi yanaongezeka katika miji mbalimbali kote Mashariki ya Kati, ikiwa ni pamoja na Jerusalem, Dubai, na Tehran.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kutokana na hatari ya kupanda kwa bei ya mafuta, hali iliyosababishwa na mzozo huo, Shirika la Nishati la Kimataifa limeamua kutoa mapipa milioni 400 kutoka kwa akiba yake ya kimkakati, ambayo bado haijazuia bei ya mafuta kupanda na kufikia zaidi ya dola 100 kwa pipa.
Israeli kujiandaa kupanua operesheni nchini Lebanon
Waziri wa Ulinzi wa Israeli Israel Katz amesema leo Alhamisi kwamba ameamuru jeshi kujiandaa kupanua shughuli zake nchini Lebanon, ambapo Israel inaendesha operesheni dhidi ya kundi la wanamgamo wa Kiislamu la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran.
“Waziri Mkuu (Benyamin Netanyahu) na mimi tumeagiza jeshi la Israel kujiandaa kupanua shughuli zake nchini Lebanon,” Katz amesema katika taarifa ya video.
“Nilimuonya rais wa Lebanon kwamba ikiwa serikali yake itashindwa kudhibiti eneo hilo na kuzuia Hezbollah kutishia jamii kaskazini na kurusha makombora nchini Israel, tutateka eneo hilo na tutafanya hivyo sisi wenyewe,” ameongeza.