
Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia, siku ya Alhamisi jioni, ameagiza wafanyakazi wa serikali wasio wa muhimu kuondoka Israel na Falme za Kiarabu kutokana na “hali ya usalama inayozorota” katika Mashariki ya Kati inayokumbwa na vita.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wafanyakazi muhimu “watabaki hko kuwasaidia Waaustralia wanaowahitaji,” ameongeza Waziri Penny Wong kwenye mtandao wa kijamii wa X, huku pia akiwahimiza Waaustralia wote “kuondoka Mashariki ya Kati ikiwa mnaweza na ikiwa ni salama kufanya hivyo.”
Kulingana na Canberra, takriban Waaustralia 2,600 kati ya 115,000 katika Mashariki ya Kati wamerudi nyumbani.