Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa
Marekani Donald Trump, amesema kuwa Marekani “Kamandi Kuu ya Marekani imetekeleza
moja ya mashambulizi yenye nguvu zaidi ya mabomu katika Historia ya Mashariki
ya Kati na kuangamiza kabisa kila shabaha ya JESHI katika kito cha taji la
Iran, Kisiwa cha Kharg”.
“Nimechagua
KUTOHARIBU Miundombinu ya Mafuta Kisiwani. Hata hivyo, iwapo Iran, au mtu
mwingine yeyote, atafanya chochote kuingilia kati Njia Huru na Salama ya Usafirishaji
Meli kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz, nitafikiria upya uamuzi huu mara
moja,” rais aliendelea.
Alitoa wito
kwa Iran kuweka chini silaha zake na “kuokoa kile kilichobaki cha nchi
yao, ambacho si kikubwa”.
Hili limetokea siku moja baada ya spika wa bunge la Iran kusema
mashambulizi kama hayo yatasababisha kiwango kipya cha kulipiza kisasi.
Moshi mnene waonekana ukipanda kutoka Kisiwa cha Kharg
lakini jeshi la Iran bado ndilo lenye kulinda kisiwa hicho: Ripoti
Shirika la habari la Iran la Fars kwa mujibu wa Al Jazeer,
limeripoti kwamba moshi mkubwa umeonekana ukipanda kutoka Kisiwa cha Kharg cha
Iran, lakini vikosi vya Iran vinaendelea kuendesha shughuli zake, kutoka huko
licha ya ya kushambuliwa najeshi ya Marekani.
Fars pia iliripoti kuwa zaidi ya milipuko 15 ilisikika
kwenye kisiwa hicho wakati wa mashambulio hayo, ikitaja vyanzo katika eneo
hilo.
Duru hizo zilisema kuwa hakuna miundombinu ya mafuta
iliyoharibiwa katika mashambulizi hayo.
Soma zaidi: