#HABARI: Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imeiagiza Wakala wa Vipimo (WMA) kuhakikisha mita zote za umeme na maji zinahakikiwa kikamilifu kabla ya kufungwa kwa watumiaji ili kulinda haki za wananchi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Deodatus Mwanyika, ametoa agizo hilo mkoani Pwani na kuitaka WMA kuimarisha usimamizi katika sekta ya ujenzi ili kupunguza malalamiko yanayotokana na vipimo visivyo sahihi vya bidhaa.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo, ameihakikishia Kamati kuwa Serikali itatekeleza maelekezo hayo kwa vitendo ili kuhakikisha usawa katika uzalishaji na uuzaji wa bidhaa.

Alisisitiza kuwa azma ya wizara ni kuona WMA inakuwa mlinzi wa mlaji kwa kuhakikisha kila bidhaa inayouzwa sokoni inaendana na thamani halisi ya fedha ya mwananchi kupitia vipimo vilivyohakikiwa.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Bw. Alban Kihulla, amewahimiza watoa huduma kuzingatia uadilifu na kuwataka wananchi kuwa mstari wa mbele kutumia vipimo sahihi.

Alibainisha kuwa uhakiki wa vipimo una nafasi kubwa katika kuleta haki na usawa baina ya mfanyabiashara na mnunuzi, jambo ambalo litaongeza imani ya jamii katika mifumo ya biashara na huduma za nishati nchini.

Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *