‎#HABARI: Majeruhi wa mwisho kati ya 11 waliosalimika kwenye ajali ya boti katika Ziwa Tanganyika, Bwana Lawi Filemoni, ameruhusiwa leo kutoka Hospitali ya Rufaa Maweni mkoani Kigoma.

Bwana Filemoni amerejea katika hali ya kawaida baada ya kupatiwa matibabu ya majeraha na mauvimu aliyoyapata Machi 13, 2026, huku wenzake 10 wakiwa tayari wameruhusiwa kwa awamu tofauti baada ya afya zao kuimarika.

Ajali hiyo ya kusikitisha ilitokea wakati watumishi hao wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wakielekea kutoa huduma za afya katika Kijiji cha Kagunga, ambapo watu saba walipoteza maisha.

Mratibu wa Huduma za Tiba wa hospitali hiyo, Dkt. Yusuph Yagasa, amethibitisha kuwa majeruhi wote sasa wako nje ya hatari, jambo linalotoa ahueni kwa ndugu na jamaa kufuatia tukio hilo lilitikisa Mkoa wa Kigoma.

Katika hafla ya kuaga miili ya marehemu kabla ya kusafirishwa kwenda mikoa mbalimbali, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro, ametoa tahadhari kali kwa wasafiri na wavuvi wanaotumia ziwa hilo.

Balozi Sirro amewasihi wananchi kufuatilia kwa karibu taarifa za mamlaka ya hali ya hewa kabla ya kuanza safari zao ili kuepuka majanga yanayoweza kuzuilika na kulinda usalama wa maisha yao.

‎Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *