‎#HABARI: Mwanamke mmoja mwenye ulemavu na mkazi wa Jiji la Mbeya anayeishi katika mazingira magumu, ametoa ombi la kipekee la kupatiwa mtaji wa shilingi elfu tano ili aweze kuanza biashara ndogo ya kumsaidia kujikimu yeye na familia yake.

Mama huyo alieleza kuwa kiasi hicho kidogo cha fedha kitakuwa mkombozi mkubwa katika maisha yake, kikimwezesha kupata mahitaji muhimu na kuepukana na hali ya duni anayokabiliana nayo kwa sasa.

Ombi hilo limetolewa mbele ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mhe. Patrick Mwulunenge, wakati wa ziara yake ya kukagua na kusikiliza kero za wafanyabiashara wadogo jijini humo.

Mbunge huyo amekutana na changamoto hiyo akiwa katika harakati za kutathmini hali ya kiuchumi ya wananchi wake, ambapo uhitaji wa mama huyo umeibua hisia za umaskini uliokithiri unaowakabili baadhi ya watu wenye mahitaji maalum katika jamii.

‎Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *