Serikali imesema itaendelea kushirikiana na sekta binafsi ili kuhakikisha huduma ya afya kwa wote inapatikana kwa Watanzania kupitia utekelezaji wa mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe, wakati wa mkutano uliowakutanisha viongozi wa Serikali, sekta ya biashara na wadau wa afya ulioandaliwa na Jukwaa la Watendaji Wakuu nchini, CEO Roundtable of Tanzania.

Dkt. Magembe amesema Serikali inaendelea kupanua miundombinu ya afya, kuimarisha huduma za uchunguzi wa magonjwa na kuboresha mfumo wa bima ili wananchi waweze kupata matibabu bila kukabiliwa na gharama kubwa.

Amesema katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imepiga hatua ambapo takribani asilimia 80 hadi 85 ya wananchi sasa wanaweza kufika kwenye kituo cha afya ndani ya umbali wa kilomita tano.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Strategis Insurance Group Tanzania, Dkt. Flora Minja, amesema uwekezaji katika afya ya wafanyakazi ni muhimu kwa kuongeza uzalishaji na ufanisi wa taasisi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa CEO Roundtable of Tanzania, Santina Majengo Benson, amesema sekta binafsi iko tayari kushirikiana na Serikali kuimarisha mifumo ya afya na kusaidia kufanikisha huduma ya afya kwa wote nchini.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *