#HABARI: Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa, Afraha Hassan, amesema Serikali inakusudia kuweka uzio wa umeme wenye thamani ya shilingi Billioni 7 katika Kata tano, zinazozunguka maeneo ya Hifadhi ya Lwafi, ambao utasadia kudhibiti Wanyama waharibifu aina ya Tembo kuharibu mazao ya wananchi.

Amesema uwepo wa uzio huo utakuwa suluhisho la kudumu katika kuwadhibiti Wanyama hao na kuwataka wananchi kuendelea kuwa na subira wakati swala hilo likiendelea kufanyiwa kazi.

Kwa upande wake Afisa Wanyamapori wilayani humo, Anod Shadrack Ngagashi, amesema Serikali inakusudia kuongeza doria katika maeneo hayo ikiwa ni pamoja na kufanya malipo ya fidia kwa wananchi wote waliokumbwa na kadhia ya kuliwa na mamba ambapo kwa mwaka 2026 watu 41 wamelipwa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *