#HABARI: Moto ambao chanzo chake hakijabainika mara moja, umeteketeza zaidi ya vibanda 20 vya wafanyabiashara katika eneo la Garden lililopo Posta, ndani ya Manispaa ya Iringa.

Moto huo ambao umetokea usiku wa kuamkia leo, umesababisha uharibifu mkubwa wa mali pamoja na bidhaa za Wafanyabiashara waliokuwa wakifanya shughuli zao katika eneo hilo maarufu kwa biashara za utalii na bidhaa za asili.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Benjamin Sitta, amesema vikosi vya zimamoto vilifanikiwa kufika eneo la tukio na kuudhibiti moto huo kwa kushirikiana na wananchi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *