#HABARI: Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa mataifa mengine yanapaswa kujiunga na juhudi za kufungua Mlango wa Bahari wa Hormuz, akisisitiza kuwa Marekani haina faida ya moja kwa moja na eneo hilo ikilinganishwa na nchi zinazotegemea mafuta yanayopita katika njia hiyo muhimu ya usafirishaji.
Akizungumza na waandishi wa habari, Trump alisema:
“Mataifa mengine yanabidi yajiunge nasi katika hii vita ya kufungua Mlango Bahari wa Homuz. Sisi Marekani hakuna tunachopata kutoka eneo hilo, hivyo wanaofaidika na mafuta ndio waje kushiriki zoezi hili. Pale panapaswa kufunguliwa na sisi tutakuwepo kuwasaidia.”
Mlango wa Bahari wa Strait of Hormuz ni moja ya njia muhimu zaidi za usafirishaji wa mafuta duniani, ukihusisha mataifa ya Ghuba na masoko ya kimataifa.
Kauli hiyo imekuja wakati mvutano wa kiusalama ukiendelea katika eneo la Mashariki ya Kati, huku jumuiya ya kimataifa ikifuatilia kwa karibu hali ya usafirishaji wa nishati na athari zake kwa uchumi wa dunia.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania