#HABARI: Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Paul Christian Makonda, amemtembelea Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, nyumbani kwake jijini Dar es Salaam na kutumia nafasi hiyo kumshukuru kwa mchango wake mkubwa kwa taifa pamoja na kulea viongozi wengi wanaolitumikia taifa katika nyanja mbalimbali.
Makonda amesema Watanzania wanaendelea kujivunia kazi na uzalendo aliouonesha Jenerali Mabeyo wakati wa utumishi wake, huku akiendelea kumuombea afya njema ili aweze kufurahia matunda ya jasho lake.
Katika mazungumzo yao, Makonda pia alizungumzia kumbukizi ya miaka mitano tangu kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, zitakazofanyika Chato mkoani Geita.
Waziri Makonda alimuomba Jenerali Mabeyo kuhudhuria kumbukizi hizo na kufikisha salamu zake, akisisitiza kuwa uzalendo, uadilifu na mapenzi ya Hayati Magufuli kwa Watanzania bado yanaendelea kuishi mioyoni mwa wengi.
Makonda amesema licha ya changamoto mbalimbali zinazoibuka katika jamii, taifa linaendelea kubaki imara na lenye mshikamano, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza maadili ya utumishi, uwajibikaji na kuwatetea wanyonge kama alivyofanya Hayati Magufuli wakati wa uongozi wake.
Powered by #MCHEZOSUPA:
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.