Nchini Mali, muungano wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, yapinga hatua ya serikali kuwataka kulipa kodi mpya kutoka kwa fedha wanazopokea kutoka kwa mashirika ya kutoa misaada kwa ajili ya miradi mbalimbali.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mashirika hayo yasiyokuwa ya kiserikali, yanahofia kuwa, utaratibu huu mpya unalenga kupunguza kiwango cha msaada wa fedha wanachpokea hasa kutoka kwa wafadhili wa Kimataifa.

Tarehe 4 mwezi Machi, Baraza la Mawaziri nchini humo, lilipitisha azimio kuwa mashirika hayo yatozwe kodi ya asilimia 10 kwa kila kiwango cha fedha wanazopokea.

Hatua hii imezua hofu ambapo viongozi wa mashirika hayo yanasema, iwapo uataribu huo utatekelezwa, huenda miradi inayowagusa wananchi wa kawaida, ikaathirika kwenye sekta ya afya na kutoa chakula kwa maelfu ya watu waliokimbia makaazi yao kwa sababu ya utovu wa usalama.

Mashirika hayo sasa yanataka mazungumzo na serikali huku yakiwa na hofu kuwa iwapo hatua hiyo itanaza kutekelezwa, wafadhili huenda wakaacha kutoa misaada hiyo kwa sababu, wanashirkiana na mashirika hayo na kufuatilia kwa kila hatua namna fedha wanazotia zinavyotumika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *