
Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya, Musalia Mudavadi anazuru Moscow nchini Urusi, katika ziara ambayo anatarajiwa kutumia kushinikiza ukomo wa raia wa nchi yake kujiunga na jeshi la Urusi, kwenda kupigana nchini Ukraine.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Akiwa jijini Moscow, Mudavadi anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa waandamizi wa serikali ya Uursi siku ya Jumatatu na Jumanne, akiwemo mwenzake Sergey Lavrov, ili kujadili suala la Wakenya kuipigania nchi hiyo nchini Ukraine.
Mudavadi anatarajiwa kutumia ziara hiyo, kuomba kurejeshwa kwa Wakenya waliorubuniwa na kujikuta wanalipigania jeshi la Urusi, baada ya kudanganya kufanya kazi zingine zenye malipo mazuri.
Jitihada hizi za Mudavadi zinakuja wakati huu, ripoi za vyombo ya ulinzi na usalama nchini Kenya, vikikadiria kuwa Wakenya zaidi ya 1,000 wamejiunga na jeshi la Urusi na wamekuwa katika mstari wa mbele kwenye vita nchini Ukraine.
Wiki kadhaa zilizopita, ndugu wa Wakenya waliokwenda nchini Urusi waliandamana jijini Nairobi, kuishinikiza serikali kuwasaidia, ili wapendwa wao kurejea nyumbani, baada ya kubainika kuwa walikuwa wanapigana nchini Ukraine.