
Milipuko kadhaa ya mabomu imetikisa mji wa Maiduguri katika jimbo la Borno, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na kusababisha idadi kubwa ya vifo na majeruhi siku ya Jumatatu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mji wa Maiduguri umekubwa na milipuko baada ya miaka kadhaa ya utulivu na kwa mujibu wa mashuhuda, walipuaji wa kujitoa mhanga ndio waliohusika na mashambulio hayo.
Milipuko hiyo ilitokea katika lango kuu ya chuo kikuu cha mafunzo ya afya cha Maiduguri, masoko mawili kwa mujibu wa Sirajo Abdullahi, mkuu wa kutengo cha serikali kinachoshughulikia majanga katika mji huo.
Mpaka sasa, haijafahamika waliohusika katika mashambulio hayo, katika eneo hio ambalo kwa miaka mingi limekuwa likishuhudia utovu wa usalama, kutokana na uwepo wa makundi yenye silaha kama Boko Haram.
Jeshi linasema liliwashambulia baadhi ya walipuaji, huku Gavana wa Borno Babagana Zulum, akisema mashamulizi hayo yanatokana na hatua ya jeshi kuendeleza operesheni dhidi ya makundi yenye silaha katika msitu wa Sambisa.
Mashambulizi haya yamejiri, wakati huu Marekani ikituma wanajeshi wake wanaokadiriwa kuwa 200 kuisaidia Nigeria, kupambana na makundi yenye simaha Kaskazini mwa nchi hiyo.