Watu kadhaa wamepoteza maisha katika mashambulio ya watu wenye silaha dhidi ya vikosi vya AFC/M23 mwishoni mwa juma lililopita huko Mugunga, katika wilaya ya Karisimbi, magharibi mwa mji wa Goma. 

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mashahidi kadhaa, kutoka katika eneo hilo milipuko ya kwanza ilisikika usiku hadi alfajiri na kutia wasiwasi wananchi wa eneo hilo utulivu ulirejea mapema alfajiri 

Asubuhi ya Jumatatu wakazi waligundua matokeo ya mapigano ya usiku huo. Maganda mengi ya makombora na risasi bado yalikuwa yametapakaa ardhini, ikithibitisha ukali wa milio ya risasi. 

Mashahidi hawa walisema kwamba zaidi ya barabara inayoelekea eneo la Kanzana, maduka kadhaa yalikuwa yameporwa. Maduka mawili makubwa ya mboga yalikuwa yameondolewa kabisa na washambuliaji. 

Idadi kamili ya vifo bado haijulikani, lakini miili miwili imeonekana, miongoni mwa waathiriwa alikuwa mwanamume aliyevaa sare za kijeshi. Miili hiyo iliondolewa jana asubuhi na gari la kubeba maiti.  Duka la magodoro lililokuwa kando ya barabara kuu katika eneo hilo liliharibiwa kabisa na moto. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *