Waziri Mkuu, Dkt Mwigulu Nchemba amesitisha kwa muda ziara yake ya kikazi katika mikoa mbalimbali nchini ili kupisha kumbukizi ya miaka mitano ya kifo cha aliyekuwa Rais, Dkt John Pombe Magufuli.
Waziri Nchemba amesitisha ziara hiuo jana jioni akiwa katika Mkoa wa Katavi ili kuhudhiria kumbukizi hiyo inayofanyika leo Jumanne Machi 17, 2026.
Akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu katika Ikulu Ndogo ya Mpanda mkoani Katavi, Waziri Mkuu alisema Serikali itaungana na Watanzania katika kumbukizi hizo za kitaifa za kumuenzi kiongozi huyo aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.
“Hautaendelea na ziara. Kama mnavyokumbuka ni siku muhimu kwa Watanzania wote, ikiwa ni kumbukizi ya miaka mitano ya aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli. Kwa heshima hiyo hatutakuwa na ziara,” amesema.
Amesema kumbukizi hizo zinafanyika kwa heshima ya kiongozi huyo aliyegusa maisha ya Watanzania wengi na kuacha historia kubwa katika uongozi na
(Feed generated with FetchRSS)