Kundi la waasi wa AFC/M23 wanaodhibiti maeneo mengi katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini limedai kwamba linawashikilia watu waliotekeleza shambulio katika eneo la Mugunga usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu na wengine wengi waliuawa, kulingana an kundi hilo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu huko Mugunga, katika wilaya ya Karisimbi, magharibi mwa Goma. Watu wenye silaha walishambulia, na vikosi vya AFC-M23 viliingilia kati na kusababisha vifo kadhaa.

Milio ya risasi ilisikika usiku. Milio mikali ya silaha nzito na nyepesi iliripotiwa kati ya saa 5 usiku na saa 7 usiku, kulingana na wakazi. Mabadilishano ya risasi kati ya washambuliaji na doria ya AFC/M23 yalisababisha vifo kati ya watu 5 na 13 miongoni mwa watu wenye silaha walioanzisha uvamizi huo, na watu 3 hadi 5 walikamatwa, kulingana na vyanzo vya ndani, ikiwa ni pamoja na vile vya AFC/M23.

Washambuliaji ni akina nani? Baadhi walikuwa wamevaa sare za kijeshi, wengine walikuwa wamevaa nguo za kiraia, lakini wote walikuwa na silaha. Maswali kadhaa bado hayajajibiwa katika hatua hii. Walitokea wapi? Na kwa nini walikuwa pale? Kulingana na vyanzo hivyo, walitokea Hifadhi ya Kitaifa ya Virunga.

Vyanzo ndani ya AFC/M23 vinaripoti visa vya uporaji. Watu hawa wenye silaha walikabiliwa na doria ya AFC/M23. Vyanzo hivi pia vinabainisha kwamba kundi hilo la washambuliaji lilikuwa linaundwa na wapiganaji wa Wazalendo na FDLR, waasi wa Kihutu wa Rwanda, ambao waanzilishi wa kundi hilo walihusika katika mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994, kulingana na Kigali.

Matukio haya yalitokea chini ya wiki moja baada ya kifo cha mfanyakazi wa misaada, raia wa Ufaransa, katika shambulio la ndege zisizo na rubani, kulingana na taarifa zilizotolewa na Umoja wa Mataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *