.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiongozi Mkuu wa Iran hayati Ayatollah Ali Khamenei alikuwa ameonya mwezi Februari kwamba hatua zozote za kijeshi za Marekani dhidi ya Iran zingezua vita vikubwa zaidi vya kieneo.

Akizungumza katika sherehe za kuadhimisha miaka 47 ya Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979 tarehe 1 Februari, Khamenei alisema: “Marekani inapaswa kujua kwamba ikiwa itaanzisha vita, mara hii itakuwa vita vya kieneo.”

Maafisa wa Iran hapo awali walikuwa wametoa maonyo kadhaa kuhusu meli na usafirishaji wa mafuta katika Mlango-Bahari wa Hormuz.

Kwa mfano, kamanda wa jeshi la wanamaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Alireza Tangsiri aliandika kwenye X mapema mwezi huu kwamba meli zinazojaribu kuvuka bahari hiyo lazima zipate kibali kutoka kwa Iran, akidai meli mbili zilipuuza maonyo na “zimenaswa”.

Iran pia imekuwa ikizishambulia mara kwa mara nchi zinazohifadhi kambi za Marekani – Qatar, Bahrain, Jordan, Falme za Kiarabu (UAE) na Kuwait – na Oman washirika wa Marekani na Saudi Arabia.

Rais wa Marekani Donald Trump alieleza kushangazwa na Iran kuwashambulia majirani zake wa Ghuba. Siku ya Jumatatu, Trump alisema “hakuna aliyetarajia” viongozi wa Iran kufyatua makombora kulipiza kisasi mashambulizi ya Marekani na Israel.

“Katika wiki mbili zilizopita, hawakupaswa kushambulia nchi hizi zote za Mashariki ya Kati,” alisema, mshirika wa BBC wa Marekani CBS anaripoti. “Hakuna mtu
aliyetarajia hilo. Tulishtuka na wakaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *