Israel, kupitia Waziri wake wa Ulinzi, Israel Katz, imetangaza kumuua Ali Larijani, mmoja wa viongozi wakuu wa Iran, na Jenerali Gholamreza Soleimani, kamanda wa wanamgambo wa Basij, kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la Israel usiku wa kuamkia leo Jumanne nchini Iran.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Mkuu wa Majeshi ameniarifu tu kwamba Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa, na Soleimani, mkuu wa kikosi cha wanamgambo cha Basij—wameuawa jana usiku,” Katz amesema katika ujumbe wa video.

Katika siku ya kumi na nane ya vita vya Mashariki ya Kati, mashambulizi ya anga ya Israel na Marekani yanaendelea katika mikuu ya Iran na Lebanon. Asubuhi na mapema Jumanne, Machi 17, milipuko kadhaa imesikika Dubai na Qatar.

Habari zaidi zinakujia…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *