Kiongozi wa muda mrefu nchini Congo Brazaville Denis Sassou Nguesso, amechaguliwa tena kuendelea kuongoza muhula wa tano, baada ya kupata asilimia 95 ya ushindi, baada ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili iliyopita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tume ya Uchaguzi imesema baada ya asilimia 95 ya kura kuhesabiwa, Nguesso, mwenye umri wa miaka 82, amepata ushindi mkubwa na kuwashinda wapinzani wake sita.

Matokeo hayo pia yamethibitishwa na Waziri wa Mambo ya ndani Zephyrin Mboulou, katika hotuba yake kwa taifa siku ya Jumanne.

Ushindi wa Nguesso ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 42, sasa unatarajiwa kuidhinishwa na Mahakama ya Katiba kabla ya kuapishwa na kuendelea kuongoza nchi hiyo ya Afrika ya Kati yenye utajiri wa mafuta.

Asilimia 84.65 ya wapiga kura walijitokeza, kushiriki kwenye uchaguzi huo, huku mtandao wa Internet ukizimwa tangu Jumapili iliyopita.

Kuelekea kutangazwa kwa ushindi wa rais Nguesso, polisi na wanajeshi walionekana wakipiga doria jijini Brazaville ambalo lilisalia mahame.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *