#HABARI: Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu Utamaduni na Michezo imeridhishwa na miradi ya Serikali inayoendelea kujengwa katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Mloganzila na kukamilika kwake kutaleta mapinduzi makubwa ya tiba nchini kwa kuwa na elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi na maendeleo endelevu ya taifa.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Husna Sekiboko wakati walipofanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali na kujionea utekelezaji wake katika chuo hicho kilichopo Mloganzila.
Akizungumza katika ziara hiyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema ziara hiyo ni chachu ya kujitathmini kile ambacho Serikali imewekeza na namna ya utekelezaji wake na kukamilika kwa miradi hiyo kutafanya eneo hilo la Mloganzila kuwa kitovu kikuu cha tiba kwa Afrika Mashariki.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.