#HABARI: Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imemhukumu kunyongwa hadi kufa Joseph Mhulilwa, dereva bajaji na Mkazi wa Mtwivila B, Manispaa ya Iringa, baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa makusudi mtoto wake wa kumzaa, Timothy Mhulilwa, wa miaka 4, kwa lengo la kujipatia utajiri.
Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Angaza Mwipopo katika kesi namba 25532 ya mwaka 2025, akibainisha kuwa upande wa Mashtaka uliwasilisha ushahidi uliothibitisha bila shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na vifungu vya 196 na 197 vya Kanuni ya Adhabu.
Ushahidi uliotolewa mahakamani ulionyesha kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 12, 2025, ambapo mshtakiwa alimuua mtoto wake, kisha kuukatakata mwili wake vipande vidogo na kuvitupa kwenye shimo la choo. Mahakama ilieleza kuwa mshtakiwa alikiri kitendo hicho, ikiwemo kuponda mifupa mikubwa kwa jiwe ili kurahisisha utupaji wa mabaki.
Baada ya kukamatwa kwake, mabaki ya mwili wa marehemu yalipatikana katika tenki la maji taka na kufanyiwa uchunguzi wa vinasaba (DNA), ambao uliothibitisha kwa asilimia 99 kuwa ni wa mtoto huyo na una uhusiano wa kibaolojia na mshtakiwa.