#HABARI: Rais wa Jamhuri ya Congo, Denis Sassou Nguesso, mwenye umri wa miaka 82, ameshinda wa uchaguzi wa urais kwa kupata asilimia 94.82 ya kura.

Matokeo hayo yametangazwa kupitia televisheni ya taifa hilo, ambapo kwa ushindi huo Nguesso ataendeleza utawala wake ambao umechukua takribani miaka 42 katika taifa hilo la Afrika ya Kati.

Katika matokeo hayo, mshindani aliyeshika nafasi ya pili, Mabio Mavoungou Zinga, amepata asilimia 1.48 ya kura.

Kwa mujibu wa televisheni ya Taifa hilo, ilieleza kuwa jumla ya wapiga kura waliojitokeza walikuwa asilimia 84.65, ingawa katika baadhi ya vituo jijini Brazzaville kulishuhudiwa idadi ndogo ya wapiga kura.

Vyama vya upinzani chini humo vilisusia uchaguzi huo, huku baadhi ya vigogo wa upinzani akiwemo Jean-Marie Michel Mokoko na Andre Okombi Salissa wakiwa gerezani kwa takribani muongo mmoja sasa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *