Iran imetuma barua saba tofauti kwa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo kuhusiana na mashambulizi ya Marekani dhidi yake kutokea katika nchi za kanda hii.

Kupitia barua hizo saba, Amir Saeid Iravani Balozi wa Iran na Mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amewasilisha malalamiko makubwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Marekani kutumia ardhi na anga za Jordan, Imarati, Bahrain, Saudi Arabia, Oman, Qatar na Kuwait dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Barua hizo zimesomeka kama ifuatavyo: Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga vikali na kutoa wito kwa nchi hizo kuheshimu ujirani mwema na kuzuia kuendelea kutumiwa ardhi zao dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Marekani na Israel Februari 28 zilianzisha vita vya kichokozi dhidi ya Iran na kumuuwa shahidi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Sayyid Ali Khamenei na makamanda kadhaa wa ngazi ya juu wa jeshi. 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia ilijibu hujuma hiyo kwa kufanya oparesheni za kulipiza kisasi dhidi ya shabaha na maeneo mbalimbali dhidi ya Israel na pia kuzishambulia kambi za kijeshi za Marekani katika eneo. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *