#MICHEZO: Bodi ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Machi 17, 2026 imetoa uamuzi mzito kwa kuinyang’anya Senegal ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 84 cha kanuni za mashindano hayo, CAF imetangaza kuwa timu ya taifa ya Senegal imepoteza rasmi mchezo wa fainali dhidi ya Morocco kwa kufungwa mabao 3-0 kwa njia ya mezani.
Kutokana na uamuzi huo, Senegal imelazimika kurejesha kombe la AFCON 2025 pamoja na medali walizokuwa wamekabidhiwa hapo awali. Kombe hilo sasa litakabidhiwa rasmi kwa Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF), ambao wametangazwa mabingwa wapya wa mashindano hayo.
Uamuzi huo umeibua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau wa soka barani Afrika, huku wengi wakisubiri ufafanuzi zaidi juu ya sababu zilizopelekea hatua hiyo kali kuchukuliwa dhidi ya Senegal.
CAF inatarajiwa kutoa taarifa ya kina zaidi kuelezea tukio hilo, huku mashabiki na wachambuzi wa soka wakifuatilia kwa karibu maendeleo ya sakata hili kubwa katika soka la Afrika.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M -Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#CapitalDigital #ITVUpdates
Follow @itvtz @radioonetanzania @capitaldigitaltanzania