Seneta wa chama cha Democratic cha Marekani amemtaja rais wa nchi hiyo kuwa ni mjinga kwa kufuata kibubusa sera za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Akikosoa sera za kuchochea vita za utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump, Seneta wa chama cha Democratic, Chris Holen, amwemwita mpumbavu kwa kutii maagizo ya Tel Aviv.
Akizungumzia mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran, Holen amesema: “Vita hivi vinaifanya Marekani na washirika wake kutokuwa na usalama zaidi. Tunashuhudia kila mara kwamba sababu (za kuanzisha vita) zinabadilika bila kuwa na lengo na mkakati wa mwisho uliowazi.”
“Tumefungua sanduku la Pandora. Wanajeshi wote wa Marekani wameuawa na raia nchini Iran, wakiwemo watoto wa shule wa kike, wameshambuliwa. Wamarekani wengi wanapinga vita hivi,” amesema seneta huyo na kuongeza: Waziri Mkuu wa Israel, Netanyahu alisema alikuwa akisubiri wakati huu kwa miaka 40. Baada ya miaka 40, wamempata rais ambaye ni mjinga vya kutosha na asiyejali wa kufanya kazi hii. Amesema maabilioni ya dola yamepotea katika vita hivi.
Wakati huo huo, Waziri wa zamani wa Vita wa Marekani amesema: Vita dhidi ya Iran vilianza na hoja kwamba tunaingia vitani ili tuweze kubadilisha serikali nchini Iran na kuwalazimisha watu wa Iran kuipindua serikali. Matokeo yake ni kwamba, iwapo serikali ya Iran haitabadilika, wao ndio watakaokuwa washindi wa vita hivi.
Sambamba na kupinga mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran, Waziri wa zamani wa Vita wa Marekani, Leon Panetta amesema: “Tunachokiona nchini Iran ni kwamba serikali imeimarika zaidi, na kwa kuchaguliwa kiongozi mpya, sasa wanahisi wana nguvu zaidi.”

Panetta amesisitiza: “Hisia hii ya kuwa na nguvu pia inatokana na uwezo wao wa kuiwekea Marekani mashinikizo.” Amekiri kwamba: “Utawala wa Iran umekita mizizi zaidi na uko imara kuliko tulivyofikiria.”