
Miongoni mwa malengo ya mashambulii ya Israel na Marekani nchini Iran Jumatano, Machi 18, yalikuwa vituo vya nishati katika mji wa kusini wa Kangan. Shambulio hilo lilisababisha moto, kulingana na televisheni ya serikali ya Iran.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Shambulio hilo liligonga vituo vya gesi vinavyotumika kuendeleza uwanja wa gesi wa South Pars, ambao unaenea hadi maji ya eneo la Iran na Qatar. Shambulio hili lilisababisha lawama kutoka kwa viongozi wa mataifa ya Ghuba, wakibainisha wasiwasi wao kuhusu kuingizwa zaidi katika vita ambavyo hawakuvitaka.
Nchi ya kwanza kujibu ilikuwa Qatar, ambayo inasimamia uwanja wa gesi wa South Pars na Iran. Shambulio la vituo vya gesi huko Kangan ni “hatua hatari na isiyowajibika,” kulingana na msemaji wa Wizara yake ya Mambo ya Nje. “Hatari” pia ilibainishwa saa chache baadaye na wanadiplomasia wa Imarati, ambao pia walibainisha “tishio la moja kwa moja kwa usalama wa nishati duniani” na kushutumu shambulio la bomu lenye “athari kubwa za kimazingira.”
Katika karibu wiki tatu za vita, viongozi wa mataifa ya Ghuba wamegundua kuwa miundombinu yao ya nishati inalengwa na mashambulizi ya Tehran, na mashambulizi dhidi ya vituo vya Iran yanaipa Jamhuri ya Kiislamu kisingizio cha kuongeza mashambulizi yake kwenye miundombinu ya majirani zake. Siku ya Jumamosi, Machi 14, baada ya mashambulizi ya Marekani kulenga Kisiwa cha Kharg, bandari kuu ya kuuza mafuta ya Iran, Tehran ilitishia kulipiza kisasi dhidi ya vituo vya mafuta vya makampuni yanayoshirikiana na Marekani.
“Pia ni mfumo wao wa maendeleo unaotiliwa shaka.” Nchi za Ghuba “hazikushauriwa, hazikuidhinisha vita hivi.” Hadi sasa zimejizuia kujiunga na muungano huo, licha ya shinikizo linaloonekana kutoka kwa Marekani, ambayo ingependa kupanua muungano huu wa pande mbili ili kujumuisha washirika wengine. Wana wasiwasi sana kwa sababu mfumo wao wa maendeleo pia unatiliwa shaka, kama vile uwezo wao wa kutekeleza miradi mikubwa, ingawa wana akiba kubwa ya kifedha. Lakini kadiri mzozo unavyoisha mapema, ndivyo bora zaidi, na wakati huo huo, ni wazi kwamba ikiwa mzozo utaisha, wanataka Marekani iwe imepiga hatua za kutosha kuelekea lengo la kupunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa mashambulizi wa Iran, ili wasijikute kesho na utawala ulioshindwa ambao bado ungekuwa madarakani na tishio kwa majirani wa Ghuba,” ameeleza François Gouyette, balozi wa zamani wa Ufaransa nchini Saudi Arabia na Falme za Kiarabu, katika mahojiano na RFI.
Taarifa hizi kutoka kwa mataifa ya Kiarabu ya Ghuba zinabainiha wasiwasi wao, lakini zaidi ya yote, kulaani kwao mashambulizi haya. Katika taarifa yake, Qatar inaishutumu Israel haswa kwa kuhusika na mashambulizi ya Jumatano.