Marekani. Sokwe wa aliyekuwa Mfalme wa Pop, Michael Jackson ametimiza miaka 43 tangu kuzaliwa kwake.
Sokwe huyo aliyezaliwa mwaka 1983 anaitwa Bubble. Kwa sasa anaishi katika hifadhi maarufu huko Florida, enzi za uhai wa MJ, alisafiri naye kimataifa na kushiriki katika ziara tofauti tofauti za mwimbaji huyo.
Kupitia chapisho lililowekwa na hifadhi hiyo la kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa sokwe huyo, wamesema ni miongoni mwa sokwe maarufu katika hifadhi hiyo na tangu awasili hapo amenawili sana.
Bubble amewahi kuwa sokwe maarufu duniani kwa kuonekana kwenye video mbalimbali za muziki, ziara za kimataifa, pamoja na vipindi vya Television. Lakini kwa sasa amekuwa akionesha uwezo wake wa kuchora katika hifadhi hiyo.
Mbali na kuchora maisha yake ya sasa yamejikita katika kusikiliza muziki wa filimbi zaidi pamoja na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kila mwaka.
Katika siku yake ya kuzaliwa Bubble hupewa zawadi mbalimbali. Zikiwemo vyakula anavyovipenda kama matunda (hasa ndizi na maapulo), keki maalum iliyotengenezwa kwa viambato salama kwa sokwe, pamoja na vifaa vya kuchezea vinavyomsaidia kujiburudisha na kuchangamsha akili.