Vikosi vya Marekani vimezindua “mfululizo wa mashambulizi makubwa” dhidi ya Iran siku ya Jumanne, “kujibu mashambulizi ya Iran dhidi ya meli tatu za kibiashara zilizopitia Mlango-Bahari wa Hormuz,” Kamandi Kuu ya Marekani (Centcom) imetangaza kwenye X. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Marekani ilitangaza kurejesha vikwazo dhidi ya mafuta ya Iran na kuanzisha “mashambulizi makubwa” dhidi ya Iran baada ya mashambulizi dhidi ya meli katika Mlango-Bahari wa Hormuz.

“Uchokozi wa Iran haukuwa na msingi, ulikuwa hatari, na ulikuwa ukiukaji wa wazi wa makubaliano ya usitishaji wa mapigano,” Centcom imeongeza, ikisema nia yake ya “kuifanya Iran ilipe gharama kubwa.”

Meli ya tatu ilipigwa na kombora lisilojulikana katika Mlango-Bahari wa Hormuz, shirika la usalama wa baharini la Uingereza UKMTO liliripoti siku ya Jumanne, siku moja baada ya shambulio kama hilo lililohusishwa na Qatar na Iran. Kutokuwa na utulivu huku katika Mlango-Bahari wa Hormuz kunasababisha bei ya mafuta kupanda tena.

Wakati huo huo jeshi la Iran limetangaza kuwa limeanzisha mashambulizi dhidi ya vituo vya kijeshi vya Marekani katika kile lilichokitaja kuwa ni jibu la mashambulizi yaliyofanywa na Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) dhidi ya zaidi ya malengo 80 kusini mwa Iran.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano, Julai 8, IRGC ilidai kuwa Marekani ilikiuka makubaliano ya kusitisha mapigano na makubaliano ya Islamabad kwa kufanya mashambulizi ya anga mapema asubuhi dhidi ya vituo vya pwani na maeneo ya kiraia katika mikoa ya Hormozgan na Mahshahr.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *