
Kutokana na mashambulizi ya makundi ya wanajihadi na hatari kubwa ya kutekwa nyara kwa raia wa kigeni nchini humo, Berlin imeamua kuwahamisha wafanyakazi wa ubalozi wake nchini Niger. Kwa taratibu zozote huko Niamey, sasa ni muhimu kuwasiliana na ubalozi wa Ujerumani huko Ouagadougou, Burkina Faso.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Nchini Niger, kuomba visa au pasipoti katika ubalozi wa Ujerumani hakuwezekani tena hadi taarifa zaidi itakapotolewa. Tangu siku ya Ijumaa, Machi 20, huduma zake za ubalozi zimesitiishwa na wafanyakazi wake wote wamehamishwa nje ya nchi kwa sababu za kiusalama, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani imetangaza katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti yake. Kwa taratibu zozote huko Niamey, sasa ni muhimu kuwasiliana na ubalozi wa Ujerumani huko Ouagadougou, Burkina Faso.
Wakati ubalozi wa Ujerumani nchini Niger pia ukikumbusha raia wake kwamba unapendekeza waondoke nchini humo, hatua hizi zinakuja chini ya miezi miwili baada ya shambulio la kigaidi karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Niamey, na takriban siku kumi baada ya kambi ya anga katika jiji la Tahoua pia kulengwa na mashambulizi.
Ujerumani sio nchi ya kwanza kuchukua uamuzi kama huo. Nchi zingine zilizotangulia, kama vile Marekani, zimeamua kupunguza uwepo wao katika mji mkuu wa Niger. Sababu zilizotajwa ni mashambulizi yaliyofanywa katika eneo la Niger na makundi ya wanajihadi, pamoja na hatari kubwa ya utekaji nyara wa raia wa kigeni.
Mwaka jana, wanawake wawili kutoka Ulaya walitekwa nyara huko Agadez na Mmarekani mmoja alitekwa nyara katikati mwa Niamey, mada ambayo iliibuliwa wiki iliyopita tu wakati wa ziara ya Nick Checker, afisa mkuu katika Ofisi ya Masuala ya Afrika katika Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
Wakati vikosi vya ulinzi na usalama vya Niger vikiwa macho kote nchini, pia vinaonekana katika maeneo kadhaa katika mji mkuu.