
Shirika la ndege la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,, Congo Airways, linakabiliwa na mgogoro mkubwa. Lilianzishwa mwaka wa 2015 likiwa na ndege nne, sasa halina ndege hata moja, kama mali yake, kwa kufanya safari za nje na dani ya nchi. Rais Tshisekedi ameona hali hii kuwa ya kutisha. Mwishoni mwa wiki hii ametaka mpango wa uzinduzi “wa kweli na uliopangwa kwa uthabiti” kwa ajli ya shirika hilo la ndege. Uamuzi huu ulifanywa baada ya uchunguzi rasmi, hasa kwa msaada wa Ukaguzi Mkuu wa Fedha.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Kinshasa, Pascal Mulegwa
Kulingana na taarifa zetu, Congo Airways kwa sasa imezorota. Ndege zake zote hazifanyi kazi kutokana na ukosefu wa matengenezo sahihi. Hata ndege zilizokodishwa hazifanyi kazi: Ndege aina ya Embraer inayofadhiliwa na Mfuko wa Kitaifa wa Hifadhi ya Jamii bado haifanyi kazi kutokana na ukosefu wa marubani waliohitimu, nyaraka za kiufundi, na vipuri. Ndege aina ya Airbus A320 iliyokodishwa kutoka kampuni ya Afrika Kusini pia inajishindwa pia kufaya kazi.
Pamoja na matatizo haya ya uendeshaji, shirika la ndege la Congo linakabiliwa na hali mbaya ya kifedha. Congo Airways imelemewa na madeni makubwa, mishahara na malimbikizo ya kodi, na imesitisha safari zote za ndege za kibiashara.
Ripoti ya uchunguzi wa pamoja uliofanywa na Ukaguzi Mkuu wa Fedha, Baraza Kuu, na Mamlaka ya Usafiri wa Anga inaonyesha matatizo makubwa katika usimamizi wa kiutawala, kifedha, na uendeshaji wa shirika hilo.
Rais Tshisekedi anabainisha mapungufu haya yanaiweka Serikali katika hatari kubwa za kisheria, kifedha, na sifa. Ili kushughulikia masuala haya, serikali imepewa jukumu la kupendekeza marekebisho kamili, ikiwa ni pamoja na usimamizi mkali wa kifedha, mifumo iliyoimarishwa ya udhibiti, na marekebisho ya utawala, ili kufufua shirika la ndege la Congo Airlines kwa njia endelevu.
Wakati huo huo, Air Congo, ikiwa na ndege zake tatu za Boeing, inapeperusha bendera ya taifa angani. Huu ni ubia na shirika la ndege la Ethiopian Airlines.