
Nchini Tanzania, wkati matokeo ya tume ya uchunguzi kuhusu vurugu za baada ya uchaguzi yakitarajiwa kutolewa Aprili 3, shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch linaongeza shinikizo. Katika ripoti iliyochapishwa siku ya Alhamisi, Machi 19, shirika hilo lisilo la kiserikali linaandika visa vya matumizi ya nguvu kupita kiasi, ikiwa ni pamoja na ufyatuaji risasi bila haki kwa raia ambao hawakushiriki katika maandamano ya Oktoba 29.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Bila idadi rasmi ya vifo katika hatua hii, HRW inatoa wito kwa mamlaka kuwa wazi kabisa kuhusu vurugu hizi na kuwataja wahusika na kuwachukulia hatua kali.
Raia kufyatliwa risasi, wakati mwingine wapita njia, ndicho ambacho Human Rights Watch inaangazia katika ripoti yake kuhusu vurugu za baada ya uchaguzi nchini Tanzania.
Hakuna idadi mpya ya vifo iliyotolewa, lakini ushuhuda maalum umekusanywa. Huko Mwanza, kaskazini mwa nchi, angalau watu saba waliuawa sokoni, kulingana na mashahidi. Kwingineko, mwanamke mjamzito alipigwa risasi na kujeruhiwa, na mwanamume mmoja aliuawa aliporudi nyumbani baada ya kupiga kura.
Kwa Human Rights Watch, inasema ufyatuaji huu wa risasi huu haujahalalishwa, ambao unakiuka kanuni za Umoja wa Mataifa. Matumizi ya nguvu za kuua yanaruhusiwa tu katika visa vya tishio la maisha. “Kwa hivyo ni muhimu kutoa mwanga kamili kuhusu vurugu hizi,” anaelezea Gerry Simpson, naibu mkurugenzi wa Kitengo cha Mgogoro katika Human Rights Watch.
Lakini mashaka tayari yanaibuka kuhusu uaminifu wa matokeo ya tume ya uchunguzi kuhusu vurugu za baada ya uchaguzi. “Tume haikutafuta vya kutosha kuwasiliana na familia ili kuelewa mazingira ya vifo hivyo, ” anaelezea. Anaongeza kwamba lazima ifanye hivyo kabla ya kuchapisha ripoti yake; vinginevyo, uchunguzi huru utahitajika.