
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mjadala wa mabadiliko ya katiba unaendelea, miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu, suala linaloonekana kuwagawa wanasiasa na wananchi wa taifa hilo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hata hivyo, wachambuzi wa siasa wanaona kuwa, mjadala huu sasa unaanza kusababisha kusahaulika kwa masuala muhimu na makubwa yanayoikumba nchi hiyo.
Kwa mujibu wa kituo cha utafiti wa siasa na uongozi cha Ebuteli nchini DRC kwa sababu za kisiasa, kati ya mwaka 2021 hadi 2025, kumekuwa na miswada 458 iliyowasilisha bungeni ni 22 ndio iliyojadiliwa tu.
Aidha, utafiti unaonesha kuwa, chama tawala bungeni kinatumia wingi wake kutanguliza maswala ya kisiasa kama kuendeleza mijadala ya mabadiliko ya katiba, baada ya kujadili masuala muhimu kama ya kiuchumi na changamoto za kiusalama, zinazowatatiza raia wa kawaida nchini DRC.
Hata hivyo, baadhi ya wanasiasa mashuhuri kama Delly Sassanga wanapinga mapendezo ya katiba kufanyiwa marekebisho kutoka kwa wanasiasa wanaomuungano mkono rais Felix Thshisekedi.
Wiki hii pia, Makamu Rais wa Pili wa Seneti Bahati Lukwebo, alijiuzulu kwenye nafasi yake, baada ya kuhusishwa na upinzani wa mabadiliko ya katiba, na kuwepo harakati za kumwondoa kwenye nafasi hiyo na wabunge.