.

Chanzo cha picha, Getty Images

Waziri Mkuu
Sir Keir Starmer na Rais wa Marekani Donald Trump wamejadili kwa njia ya simu umuhimu
wa kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz katika mzozo unaoendelea Mashariki ya
Kati.

Msongamano
wa meli kupitia njia hiyo – mojawapo ya njia zenye shughuli nyingi zaidi za
meli duniani – umepungua kwa takriban 95% tangu vita vya Iran vianze tarehe 28 mwezi
Februari.

Msemaji wa serikali
ya Uingereza alisema viongozi hao “walikubaliana kwamba kufungua tena
Mlango-Bahari wa Hormuz ilikuwa muhimu ili kuhakikisha utulivu katika soko la mafuta
duniani” wakati wa mazungumzo siku ya Jumapili jioni.

Haya
yanajiri huku Sir Keir akitarajiwa kuongoza mkutano wa Baraza la Mawaziri, ambao
utahudhuriwa na gavana wa Benki Kuu ya Uingereza Andrew Bailey siku ya Jumatatu,
kujadili athari za vita hivyo kwa gharama ya maisha.

Msemaji wa Uingereza
alisema Sir Keir na Trump “wamekubaliana kuzungumza tena hivi
karibuni”.

Iran
imefanikiwa kufunga mlango-bahari huo tangu Marekani na Israel ziliposhambulia
nchi hiyo tarehe 28 Februari.

Takriban 20%
ya mafuta na gesi asilia duniani kwa kawaida hupitia njia hiyo, na bei za
mafuta duniani zimepanda kutokana na vita, huku mafuta ghafi yakipanda kwa 45%
hadi $106 kwa pipa.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *