
Iran imemteua Mohammad Bagher Zolghadr, kamanda wa zamani wa Walinzi wa Mapinduzi na mfuasi wa marehemu Ali Larijani, kuchukua nafasi yake kama mkuu wa Baraza kuu la usalama wa taifa, televisheni ya serikali imeripoti leo Jumanne Machi 24, 2026.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ali Larijani, mwanasiasa mashuhuri na nguzo ya Jamhuri ya Kiislamu, aliongoza chombo cha usalama cha juu zaidi cha Iran hadi kifo chake wiki iliyopita katika mashambulizi ya anga ya Israel huko Tehran.
Hayo yanajiri wakati Iran ilitishia siku ya Jumatatu, Machi 23, kuweka mabomu ya majini katika Ghuba ikiwa pwani yake itashambuliwa. Kabla ya hapo, Iran ilitishia kushambulia miundombinu muhimu katika Mashariki ya Kati na kufunga kabisa Mlango-Bahari wa Hormuz ikiwa mitambo yake ya umeme italengwa, ikijibu makataa ya Rais wa Marekani Donald Trump.
Habari zaidi zinakujia…