NAIROBI – Serikali ya Kenya na wadau wa maendeleo wanakabiliwa na changamoto kubwa katika ufadhili wa misaada ya kibinadamu na miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo kame), kwa mujibu wa ripoti mpya. Ripoti hiyo iliyochapishwa na taasisi ya Institute of Public Finance (IPF) inaangazia pengo kubwa la ufadhili pamoja na hitaji la kuimarisha mifumo ya kusaidia jamii za maeneo hayo kukabiliana na majanga.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa utafiti huo, maeneo ya ASAL nchini Kenya yamekuwa yakitegemea zaidi misaada kutoka kwa wafadhili wa kimataifa badala ya rasilimali za ndani. Hali hii inaathiri uwezo wa serikali za kaunti na jamii husika kupanga na kutekeleza miradi ya muda mrefu ya kukabiliana na majanga.
Ripoti inaonyesha kuwa licha ya uwepo wa mifumo ya kitaifa ya kukabiliana na ukame na majanga, fedha zinazotengwa bado hazitoshi kukidhi mahitaji yanayoongezeka kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Athari kwa wananchi wa ASAL
Maeneo ya ASAL, ambayo yanajumuisha kaunti 23 nchini Kenya, ndiyo yaliyoathirika zaidi na ukame, uhaba wa chakula na migogoro ya rasilimali.Mamilioni ya watu huathirika kila mwaka na huhitaji msaada wa kibinadamu.
Mbali na ukame, wananchi katika maeneo hayo pia hukabiliwa na changamoto za ukosefu wa maji, huduma za afya na miundombinu duni, hali inayoongeza hatari ya majanga ya kibinadamu.
Ripoti hiyo pia inasisitiza umuhimu wa kuunganisha nguvu nguvu za maamuzi na rasilimali kwenda katika ngazi za kaunti na jamii.
Hatua hizi zinalenga kuhakikisha kuwa jamii zinakuwa na uwezo wa kujibu majanga kwa haraka na kwa njia endelevu.
Mwelekeo wa baadaye
Wataalamu wanasema bila mabadiliko ya haraka katika sera na ufadhili, hali ya kibinadamu katika maeneo ya ASAL inaweza kuendelea kuwa mbaya zaidi, hasa kutokana na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabianchi.
Mashirika ya kibinadamu yanaendelea kutoa msaada, lakini pia yanasisitiza umuhimu wa kuwekeza katika suluhisho za muda mrefu zitakazopunguza utegemezi wa misaada ya dharura.