Siku moja baada ya rais Donald Trump kutangaza kuwa Marekani inasitisha kushambulia vituo vya nishati vya Iran kwa siku tano ili kupitisha mazungumzo, jeshi la Marekani na Israeli limeendeleza mashambulio katika maeneo mbalimbali ya Iran, ambayo pia imeshambulia Israel likiwemo jiji la Tel Aviv.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Licha ya mashambulio hayo, Marekani inasema mazungumzo yaliyopagwa yataendelea lakini hali ni tete. Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif, amesema nchi yake iko tayari kuwa mwenyeji wa mazungumzo hayo.

Rais Trump ameendelea kusisitiza kuwa Iran kwa sasa inataka suluhu baada ya kushambuliwa.

Hata hvyo, Tehran nayo imeendelea kukanusha kuwa mazungumzo hayo yanaendelea, na kutaja tangaoz la Trump kama habari za uongo huku Mohammad Baqer Zolqadr akiteuliwa kuwa Mkuu mpya wa Baraza la usalama, akichukua nafasi yake Ali Larijani, aliyeuwa wiki iliyopita.

Wakati kukiwa na matumaini hayo ya mazungumzo, jeshi la Marekano nalo limeendleza kushambumia miji ladhaa ya Iran, ambayo nayo imerusha makoùmbora yake jijini Tel Aviv na kusababisha majeraha, lakini pia ikalenga Bharian, Saudi Arabia na Kuwait.

Naye Waziri wa Ulinzi wa Isreal,  Israel Katz, amesema jeshi la nchi yake linalenga kudhibiti Kusini mwa Lebanon, karibu na mto Litani, mpango ambao Ufaransa inatoa wito kwa Israel kuachana na harakati hizo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *