
Marekani imetangaza mwishoni mwa wiki iliyopita, kupitia balozi wake katika Umoja wa Mataifa, Mike Waltz, nia yake ya kufanya mapitio ya kimkakati ya misheni kadhaa za Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Kura ya Maoni katika Sahara Magharibi (MINURSO).
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ingawa Washington awali ilitaja sababu za kifedha, marekebisho haya yanahusiana kwa karibu na majadiliano yaliyoanzishwa katika wiki za hivi karibuni na Morocco, Algeria, Mauritania, na Polisario Front kuhusu utawala wa Sahara Magharibi.
Miongoni mwa hoja zilizowasilishwa kwa Bunge na mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Mike Waltz, kwa ajili ya kupanga upya misheni za Umoja wa Mataifa kama vile MINURSO, ni pamoja na gharama kubwa inayoonekana na ufanisi mdogo wa misheni hizi za muda mrefu.
“Ni jambo moja kukomesha uhasama kati ya pande hizo mbili. Lakini hilo haliwezi kuwa kisingizio cha kushindwa kufikia azimio la kisiasa,” alitangaza.
Mapitio haya ya kimkakati ya MINURSO yanaonyesha nia ya kuweka kipaumbele hatua za moja kwa moja za Marekani kuhusu Sahara Magharibi, iliyoanzishwa katika wiki za hivi karibuni kupitia mikutano kadhaa huko Madrid na Washington, kulingana na Khadija Mohsen-Finan, mtaalamu wa Maghreb aliyewasiliana na RFI.
“Mikutano kadhaa tayari imefanyika ili kufafanua upya misheni ya MINURSO, ” amesema mtaalamu wa Maghreb Khadija Mohsen-Finan huku akibainisha kwamba Marekani inaoneakan imeanza kupunguza msaada wake kwa MINURSO
Mtaalamu huyo wa masuala ya siasa anabaini kwamba “Marekani inachukua nafasi kabisa ya Umoja wa Mataifa. Jukumu la Misheni hii lazima libadilishwe kutokana na nia ya Donald Trump ya kuvuruga hali ilivyo kuhusu suala la Sahara Magharibi.”
Mustakabali wa MINURSO utajadiliwa katika wiki zijazo katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.