
Msaada wa maendeleo kwa kubadilishana na rasilimali za madini: Ikulu ya White House imeahidi kuwekeza dola milioni 320 katika mfumo wa afya wa Zambia mwaka wa 2026, ikiwa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika itasaini makubaliano ya pande mbili kuhusu, miongoni mwa mambo mengine, rasilimali za madini za nchi hiyo. Jaribio hili kali la Ikulu ya White House la kupata udhibiti wa shaba na kobalti limeshutumiwa kama usaliti na wanaharakati wengi wa sekta ya afya.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Johannesburg, Valentin Hugues
Wafanyakazi wa afya wameshtuka na wanalaani kile wanachokiona kama usaliti wa kifedha usiokubalika. Asia Russell anaongoza shirika lisilo la kiserikali la Health Gap, ambalo lilitangaza hadharani itfaki ya makubaliano kati ya Marekani na Zambia.
“Ukiangalia hati ya makubaliano tuliyochapisha wiki iliyopita kwenye tovuti yetu, utaona wazi kwamba, isipokuwa nchi hiyo ijitoe kuweka masharti ya usaidizi wake kuhusu upatikanaji wa rasilimali zake za madini kwa Marekani, makubaliano yanayohusiana na kufadhili mapambano dhidi ya VVU, kifua kikuu, malaria na matatizo ya afya ya umma ni batili.”
Kwani, sambamba na hayo, Ikulu ya White House inajaribu kusaini makubaliano ya pande mbili kuhusu rasilimali za madini ya Zambia. Zambia ina utajiri wa shaba na kobalti, anaeleza Asia Russell. “Sisi si wajinga; tunajua kwamba mazungumzo ya udanganyifu au yasiyo na ulinganifu mara nyingi hutokea. Lakini katika masuala ya afya, magonjwa hayana mipaka, na udanganyifu katika eneo hili ni wa ajabu sana kwa sababu unapodanganya katika sekta ya afya, unawafanya watu wateseke.”
Zimbabwe, nchi jirai, hivi karibuni ilikataa makubaliano kama hayo na Washington kwa msingi kwamba misaada ya maendeleo haiwezi kutumika kama njia ya uchimbaji wa kimkakati.