Rais Samia: Taifa limepoteza kiongozi shupavu, mahiriRais Samia: Taifa limepoteza kiongozi shupavu, mahiri

DAR ES SALAAM — Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema taifa limepoteza kiongozi shupavu, mahiri na mzalendo kufuatia kifo cha William Vangimembe Lukuvi.

Katika salamu zake za rambirambi, Rais Samia alisema Lukuvi alikuwa mtumishi wa umma mwenye uzoefu mkubwa aliyelitumikia taifa kwa uadilifu, weledi na kujitolea, huku mchango wake katika maendeleo ya nchi ukiendelea kukumbukwa.

Ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, familia ya marehemu, wananchi wa Jimbo la Isimani pamoja na Watanzania wote.

Rais Samia ameomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *