Wamiliki wa magari jijini Kinshasa nchini DRC, kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita, wanashuhudia uhaba wa mafuta kwenye vituo vya kuuza bidhaa hiyo, huku misururu mirefu ikishuhudiwa hali inayodaiwa kuchangiwa na vita mashariki ya kati.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Maderva wa uchukuzi wa umma na wamiliki wa magari binafsi wamekuwa wakipanga foleni kwenye vituo vya gesi.

“Bei ya nauli imepanda kabisa, madereva wanasema hakuna mafuta.Watu wanaanza kwenda kazini kwa miguu na hata wanafunzi kuchelewa shuleni.” Walisema baadhi ya raia wa Kinshasa.

Ilikupata mafuta, madereva wamelazimika kukita kambi kwa saa kadhaa kwenye vituo vya mafuta. Lyda Chris ni dereva.

Nishida sana kupata mafuta ya gari. Ukienda kituo cha gesi utashinda mchana wote huko, lakini hatuelewi nini tatizo, wengi wemesema ni kutokana na vita vya Iran ndiyo ina sababisha uhaba huu wa mafuta, Serikali nayo haisemi chochote. Bila mafuta hatujuwi tutafanya vipi kazi.” Alisema Lyda Chris ambaye ni dereva

Emery Mbachi, mwenyekiti wa Chama huru cha wauzaji wa mafuta DRC, amesema changamoto hii huenda ikawa mbaya zaidi  kutokana na vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati.

Leo Mashariki ya Kati kuna tatizo halisi lililojitokeza na linaathiri dunia nzima. Inabidi kuweka akiba ya mafuta kuwapa watumiaji kukabiliana na tatizo lililopo.” Alieleza Emery Mbachi.

Naye waziri anayehusika na masuala la nishati nchini DRC Acacia Bandubole, amekanusha madai hayo uhaba wa mafuta kwenye taifa lao. 

Watu wafahamu kwamba hakuna uhaba wa mafuta nchini. Umati huo wa watu kwenye vituo vya gesi ni kutokana na tatizo la usawa wa kiuchumi, vifaa na kifedha.”

Freddy Tendilonge Kinshasa RFI Kiswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *