
Umoja wa Mataifa umependekeza mpango wa misaada ya dharura kwa Cuba, ikiwa ni pamoja na uwasilishaji wa mafuta, kama sehemu ya majadiliano na Marekani kuhusu idhini ya uagizaji wa bidhaa za kibinadamu, afisa wa Umoja wa Mataifa amesema siku ya Jumatano, Machi 25. Mpango huu unakuja huku Shirika la Afya Duniani likiona hali ya afya kisiwani humo kuwa ya kutisha.
Imechapishwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Francisco Pichon, mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Cuba, ameelezea kwamba mpango huu wa dola milioni 94.1 ulipendekezwa ili kudumisha huduma muhimu kwa watu walio katika mazingira magumu zaidi nchini na “kuokoa maisha” ya watu. “Ikiwa hali ya sasa itaendelea na akiba ya mafuta nchini humo ikiisha, tunafia kuzorota kwa kasi hali ya kibinadamu, na hatari ya watu kupoteza maisha,” aliliwaambia kundi dogo la waandishi wa habari, ikiwa ni pamoja na shirika la habari la AFP.
Mpango huo uliwasilishwa Machi 24 kwa wanadiplomasia na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa. Ni mwendelezo wa majibu ya Umoja wa Mataifa kwa uharibifu uliosababishwa na Kimbunga Melissa, ambacho kiliikumba Cuba mwezi Oktoba mwaka uliyopita, na kinajumuisha athari za kibinadamu za mgogoro wa sasa wa nishati, uliozidishwa na kizuizi cha mafuta kilichowekwa na Marekani shidi ya kisiwa hiki cha kikomunisti tangu Januari.
Mpango unaowezesha ufuatiliaji wa misaada
Kulingana na Francisco Pichon, “uwezekano na utekelezaji wa mpango huu ni wazi unategemea suluhisho za mafuta.” Kwa lengo hili, Umoja wa Mataifa unapanga “mfumo wa ufuatiliaji wa mafuta” ili kuhakikisha “kwamba unaelekezwa kwa huduma muhimu na bora zilizopewa kipaumbele katika mpango huo,” alielezea. “Suluhisho zote zinazingatiwa, ikiwa ni pamoja na ushirikiano na sekta isiyo ya kiserikali,” aliongeza.
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wameshindwa kwa kiasi kikubwa kufanya misheni katika maeneo mbalimbali, na mashirika ya Umoja wa Mataifa yanajitahidi kupata shehena za misaada kutoka viwanja vya ndege vya Havana. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alionya mwezi uliopita kwamba Cuba iko hatarini kukumbwa na “mgogoro wa kibinadamu” ikiwa itanyimwa ufikiaji wa mafuta.
Wacuba wanapitia hali ngumu ya kukatika kwa umeme mara kwa mara ambako kunaweza kudumu zaidi ya saa 20, na kukatika kwa umeme mara mbili kulitokea wiki iliyopita pekee. Rais wa Cuba Miguel Díaz-Canel ameweka hatua mbalimbali za kuhifadhi mafuta, ikiwa ni pamoja na mgao mkali.
“Hali ya afya inatia wasiwasi”
Mkurugenzi Mkuu wa WHO alisema mnamo Machi 25 kwamba hali ya kiafya nchini Cuba ilikuwa “ya kutia wasiwasi sana,” huku vikwazo vya mafuta vya Marekani vikizidisha mgogoro wa nishati kisiwani humo. “Afya lazima ilindwe kwa gharama yoyote na kamwe isiwe chini ya udhibiti wa siasa za kijiografia, vizuizi vya nishati, na kukatika kwa umeme,” alibainisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus kwenye mtandao wa kijamii waX.
“Hali nchini Cuba inatia wasiwasi sana, kwani nchi hii inajitahidi kudumisha huduma za afya wakati wa msukosuko mkubwa, na kusababisha uhaba wa nishati unaoathiri afya,” aliongeza.
Mfumo wa uzalishaji umeme wa Cuba unaozeeka husababisha kukatika kwa umeme kila siku ambao unaweza kudumu hadi saa 20. Kisiwa hicho kinakosa mafuta yanayohitajika ili kuzalisha umeme wake.
Tangu Marekani ilipomwondoa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, mshirika mkuu wa Cuba, mnamo Januari 3, uchumi wa kisiwa hicho umeathiriwa zaidi, huku Rais wa Marekani Donald Trump akiendelea kushikilia kizuizi cha mafuta. Hakuna usafirishaji wa mafuta ulioingizwa kisiwani tangu Januari 9, na kuathiri sekta ya umeme na kulazimisha mashirika ya ndege kupunguza safari za ndege kwenda Cuba—pigo kubwa kwa sekta muhimu ya utalii.
Hospitali za Cuba ziko katika hali ngumu
Tedros Adhanom Ghebreyesus alinukuu ripoti za vyombo vya habari kwamba hospitali za Cuba zimejitahidi kudumisha huduma zao za dharura na huduma za wagonjwa mahututi. “Maelfu ya taratibu za upasuaji zimeahirishwa katika mwezi uliopita, na watu wanaohitaji huduma, kuanzia wagonjwa wa saratani hadi wanawake wajawazito wanaojiandaa kujifungua, wako hatarini kutokana na ukosefu wa umeme wa kuendesha vifaa vya matibabu na kudumisha mnyororo baridi wa chanjo,” alisema.
“Hospitali za Cuba, kliniki, na magari ya wagonjwa zinahitajika sasa zaidi ya hapo awali na lazima ziungwe mkono,” aliongeza. Mbali na kukatika kwa umeme kila siku, bei za mafuta zimepanda, usafiri wa umma ni mdogo, na taka zinarundikana kwa sababu malori ya taka hayafanyi kazi tena.