Katika mahojiano na televisheni ya kitaifa, Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Abbas Araqchi, aliweka wazi kuwa mapendekezo ya Marekani ya kumaliza vita yanapitiwa na mamlaka ya juu jijini Tehran.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Licha ya kuthibitisha kwamba nchi yake inapitia mapendekezo ya Marekani, alisistiza kuwa ujumbe wanaoupokea kupitia kwa wapatanishi hauwezi kuchukuliwa kama mazungumzo.

Matamshi yake Araqchi yalionyesha nia ya Tehran kufanya mazungumzo ya kumaliza mapigano iwapo marsharti yake yatazingatiwa.

Alisisitizia msimamo wa Tehran kwamba ujumbe wanaopata kutoka kwa Marekani kupitia kwa wapatanishi sio mazungumzo kama inavyodaiwa na Marekani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Israeli Channel 12, mpango wa Rais Trump uliowasilishwa hwa Iran kupitia kwa Pakistani unajumuisha, Shuguli katika vinu vya nyukilia vya Natanz, Fordow na Isfahan zitasitishwa na vinu hivyo kuharibiwa.

Shirika la nishati ya Atomiki (IAEA) litapewa nafasi ya kufuatilia kwa uwazi shughuli zinazohusiana na nyukilia nchini Iran miongoni mwa mengine.

Soma piaNini kipo kwenye mapendekezo ya Trump kwa Iran kumaliza vita?

Licha ya White House kutoweka wazi mapendekezo yake, imetishia kuzidisha mzozo iwapo Iran haitoyazingatia.

Iran imeshambulia nchi zilizo na kambi za kijeshi za Marekani na kufunga Mlango-Bahari wa Hormuz.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *