Nchini Sudan, wanamgambo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) wametangaza mnamo Machi 24 kwamba wameuteka mji wa al-Kurmuk katika Jimbo la Blue Nile, kusini mashariki mwa nchi, kwenye mpaka na Ethiopia. Wanaungwa mkono na Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Sudan-Kaskazini (SPLP-N), kundi la waasi linaloongozwa na Abdelaziz el-Hilu.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Sudan lilijiondoa hadi kwenye kambi yake ya nyuma huko Damazin, mji mkuu wa Blue Nile. Kutekwa kwa mji huu wa kimkakati kumefufua shutuma kwamba Ethiopia inahusika katika vita nchini Sudan kwa kusaidia kijeshi RSF. Mapigano yalianza Machi 22 na yameiruhusu RSF kuteka miji mingine kadhaa.

Hali hii inabadilisha usawa wa nguvu katika Jimbo la Blue Nile kusini mashariki mwa Sudan. Hii inawakilisha maendeleo ya kimkakati kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), lakini inasababisha Ethiopia kuonyooshewa kidole cha lawama. Serikali ya Blue Nile ilisema katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba vikosi vinavyoendesha shambulio hilo “vilitoka ndani ya eneo la Ethiopia” na kwamba “magari ya kijeshi yaliwasili kutoka uwanja wa ndege wa Arosa.”

Wapiganaji hawa “wanaungwa mkono na Ethiopia,” Gavana wa Blue Nile Abdelatty al-Faki aliliambia shiika la habari la AFP, akirudia kauli zilizotangulia. Alilaani “uvamizi,” akibainisha kuwa raia wameanza kukimbilia mji mkuu, Damazin. Raia wengine wamekimbilia Ethiopia.

Afisa wa jeshi aliyeko katika uwanja wa mapigano alithibitisha kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba jeshi liliwakamata wapiganaji 75 kutoka kwa vikosi vya Joseph Toka, vya Kundi la 147 la Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Sudan-Kaskazini (SPLP-N), ambao walitoka Ethiopia kutekeleza shambulio hilo.

Mustapha Tambour, mkuu wa kikosi kinachoshirikiana na jeshi, alifichua kuwepo kwa kambi hii mnamo mwezi Oktoba 2025. Vyanzo kadhaa vinadai kwamba wapiganaji elfu chache walifunzwa huko kulenga Blue Nile. Madai haya yaliwasilishwa kwa Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Misri, ambaye alinukuu “ripoti zilizoandikwa kwamba majirani wa karibu wa Sudan walikuwa wameanzisha kambi za kutoa mafunzo na kuwapa silaha RSF.”

Kambi ya kijeshi katika eneo la Ethiopia

“Vyanzo” vilivyothibitishwa vinaripoti kuwepo kwa kambi ya kijeshi huko Menge, katika eneo la Benishangul-Gumuz ndani ya eneo la Ethiopia. Eneo hili liko karibu na uwanja wa ndege wa Arosa. Picha za setilaiti zilizochambuliwa na shirika la habari la AFP zinaonyesha kazi ya ujenzi inayofanywa katika kambi hii na katika uwanja wa ndege ulio karibu. Kulingana na akaunti maalum ya ujasusi ya AfriMEOSINT, ndege za mizigo kutoka Falme za Kiarabu mara nyingi hutua hapo, licha ya UAE kukanusha. Addis Ababa inaendelea kukanusha kutumika kama kambi ya usaidi ya Vikosi vya RSF.

Kama eneo la kimkakati la kweli, Kurmuk iko kwenye ardhi ya juu katika eneo muhimu linalounganisha maeneo kadhaa ya Sudan. Pia inaunganisha Sudan na Ethiopia na Sudan Kusini. Kurmuk iko karibu na bonde la Bwawa la Roseires. Ina utajiri wa maliasili, haswa maji. Nafasi yake inaruhusu udhibiti wa njia kati ya Jimbo la Blue Nile na Jimbo la Sinnar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *