Dar es Salaam. Roja Boy. Mwanangu kitambo. Toka Wailes Temeke, Mabibo Jeshini, Sinza Mori mpaka sasa maisha yanaendelea. Langu lake na lake ni langu, tusichoshea ni madem tu na nguo. Hatutupani kiboya kwa mishe za kupita.

Desemba iliyopita mwana aliishi kinyoge sana. Baada ya pisi kali yake Shaymaa kumtema jumla kisa ni bishoo mmoja wa Goba. Jamaa dizaini ‘anapushi’ ‘krauni asilete’, vinjuka na ‘fomu siksi’ za kutosha. Dem kawaka kamtosa Roja kinoma noma. 

Ikumbukwe Roja alijiweka kwa huyu dem, baada ya kutoswa na dem wake wa kitambo Mwajei wa Kurasini Ufundi. Daah, mwaka mmoja mbele anapigwa chini tena na dem mwingine. Mchizi akajihisi hafai tena kuwepo chini ya dunia hii ya Trump na ‘AI’.

Harakati zake zikasizi. Akawa ni mtu wa kuuchuna kama kavuta bange za Naliendele, stresi tupu kama bwege hivi. Lakini mwana huku huku mara paa juzi kapiga mshindo wa hatari. Treni refu la mkeka liboooom.

Hivi tunavyoongea Roja kasogea kwa Madiba kuoga kwanza. Zile shati za kwenye isidingo na za wachambuzi wa Supa Spoti ndo anazitaka. Kadondoka hapo mjini ‘Jobegi’ kibabe sana kama Chris Brown. Unajua tena.

Roja alirithi kimo kwa mamaake. Ujue Bi. mkubwa wake ni mrefu ana asili ya Tabora Mnyamwezi. Basi Roja huwa anajikuta Jay Z au Kobe. Lakini pamoja na urefu na ‘siksi paki’. Pisi zinamtema deile kama ‘bigijii’.

Akirudi madem zake waliomtosa watajuta. Namjua Roja malipizi yake. Hivi hapa naongea mwana kaagiza ‘krauni’ tayari Japenga. Ni wiki mbili zijazo mzigo unatua Bandali Salama, hiyo misele’ake siipatii picha. Tutajuta.

Roja kaagiza mashine kama ile ile aliyoporewa Shaymaa wake. Ni kama aliporwa dem ili akasirike kisha afanye malipizi. Ujue Roja ni bishoo aliyekosa matunzo, leo hii kapiga kama 50 milioo. Kaka utamuambia nini? 

Oyaa wanangu. Kuna majembe yanalisha mtaa ‘dei tu dei’. Kiroho safi wana ‘spridi’ mikeka ‘frii’ ile ‘ki-waifai’. Kuanzia insta, tikitoku, fesibuku, twitani na wasapu zao zina chaneli. Unyama ni mwingi sana mwaisa, na hii ni zaidi ya mapendo.

‘Striti’ ni ‘jam’ ya mikeka ‘naudeizi’ haichaniki tena. Wanaweka treni na behewa zake na kitu ni tiki tu na ‘maodsi kibao. Ni akili kubwa hizi, zimeachana kuunda meli na ndege zinacheza na namba ‘deile’ na mdosi analia kiroho mbaya.

Kila wiki masela shazi wanaagiza na kuisogeza mikoko uani kwao. Wakamaria na ‘krauni’ kama Big Man Snop na bange. Iko hivi kila wiki kuna watu wanaingiza pesa ndefu kwa akili za mtu tatu kama milioni tatu. Oya siyo poa.

Mdosi anavyojichanganya naye, anazima ‘keshi auti’. Hapo wana ndo wanambabua kama mahindi ya Mporoto. Akiamini ‘keshi auti’ inamtia hasara, kumbe ni mikeke ilyisukwa na akili kubwa. Mwisho anaosuka parefu.

Akiendelea na hizo mishe mdosi atarudi Mumbai. Wana wanapiga mawe siyo kitoto kama vile Geita na Mirerani tu. Na kina Taivana na wenzake walivyo na moyo wa kirasta fari, mikeka wanaanika hadharani. Mitaa inavimbiwa.

Juzi tu msela wetu Prolific katoa mkeka wa ‘odsi’ 160. Mwendo wa basketball maana ligi maduniani zimesimama kulisha udwanzi wa ‘intaneshino breki’. Na ‘odsi’ 160 zote keka limetoa “pipo’ zimepiga mpunga kinoma.

Hakuna sababu ya kukaba tena, hakuna sababu ya kulelewa na mama yenye ngoma mjini. Kama wana wanagawa upendo namna hii mnataka nini tena masimela? Acheni ‘stresi’ za bahasha za kaki na vyeti vya kuombea ajira.

Ruka na wanetu ‘deile’ wapo na wanagawa mapendo kimikeka. Kazi yako ni kuwaombea kazi ya akili zao ibarikiwe kisha tia zako mpunga sikilizia mawe. ‘Lavu’ ya namna hii hupatikana kwenye mioyo safi pekee.

Na wenye mioyo safi watauona ufalme wa ‘Saa Godi’. Achaneni na wanetu walitoboa, wakiziona kitaa sura zetu zinawaboa. Hao waacheni na mioyo ya kifarisayo,  turuke na masela wetu hawa na tuwaombee uzima na afya safi.

Hakuna namna tena wanangu, kila mchongo hattarishi mjini. Tafuta mtaji achana na bapa hata wiki moja. Nata na biti la Taivina ‘deile’, weke jero, kesho buku. Taratibu ‘suuni’ utaanza kumpasua mdosi pesa mingi mingi kama wao.

Hawa ndo wa kuwatolea macho, kuwaombea kwa Mungu. Wapo na mtaa, wanalisha mtaa, wana wanalila kodi za nyumba na ada za madogo kwa sababu ya hawa masela. Hawa ni masela tu kama vile Petro, Zakayo na Yakobo.

Ni vijana wa Kitanzania, ambao mioyo yao imebarikiwa na kujaa upendo wa Agape. Wana ‘lavu na striti’, ‘lavu na pipo’, ‘lavu na gem’ na wana hela of coz. Kimsingi ni wahuni walioishi kiinjilisti na utu wa kiimani haswa. Upendo.

Wakati Magu alileta na kujenga treni ya umeme. Hawa wanatupa matreni ya mikeka ili tupige pesa tukapande treni la umeme. Kwa kweli kuliko kuwaombea wahuni wa kisiasa ni bora niwaombee hawa masela. Maana wanaugusa mtaa ‘streiti’.

Wiki mbili nyumba Sati aliweka treni la ‘oddsi’ 83. Watu wakapiga pesa. Taivina akaleta ‘rollova’ ya ‘faivu deizi’ wana wakapiga pesa. Funga kazi kwa Prolific na ‘oddsi’ zake 160 za basketi. Ni kwereee. Oyaaaa siyo poa, ni mwendo wa mateka kwa mdosi!

Huo mkeka wa ‘odsi’ 160 ndio uliyomtoa na mwanangu Roja. Wacha masela tuvimbe kitaa na mgao wa mikeka kutoka kwa wana wenye ‘lavu’ na mtaa. Oya Taiv, Sati na Pro, Pasaka hiyo lisheni mitaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *