Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) ametuma salamu za rambirambi kwa wakurugenzi wa Televisheni za Al-Manar na Al-Mayadeen za Lebanon kufuatia hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuwauwa kwa makusudi waandishi habari wa vyombo hivyo habari kusini mwa Lebanon.

Katika jumbe mbili tofauti zilizoelekezwa kwa wakurugenzi wa Televisheni za Al-Manar na Al-Mayadeen, Dakta Peyman Jebelli amepongeza na kutoa mkono wa taazia kufuatia kuuliwa shahidi Ali Shoaib, ripota wa Televisheni ya Al Manar na kuandika kuwa: Katika miaka kadhaa ya mapambano ya jihadi, kamera na sauti ya shahidi huyo vilifichua ukandamizaji wa adui Mzayuni, na misimamo yake ya ujasiri ilitoa changamoto kwa mashine ya vita ya watenda jinai.

Jebelli amepongeza na kutoa pole kwa niaba ya wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) kutokana na mauaji hayo ya kikatili na kusema anataraji kuwa kuuawa shahidi ripota huyo kutakuwa mwanzo wa ushindi dhidi ya maadui wa Kimarekani na Kizayuni.

Peyman Jebelli 

Wakati huo huo, Mkuu wa IRIB ametuma ujumbe kwa mkurugenzi wa Televisheni ya  Al-Mayadeen akitoa mkono wa taanzia kwa mauaji ya mwandishi wa televisheni hiyo Fatima Ftouni . Amekitaja kitendo hicho cha jinai kuwa jitihada za kuuwa neno la ukweli na kitendo kilicholenga kunyamazisha sehemu ya mapambano ya haki dhidi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Peyman Jebelli amemuomba Mwenyezi Mungu aviwezesha vyombo vya habari vya Muqawama katika kukabiliana na maadui  wa haki na ubinadamu hasa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Fatima Ftouni na mpiga picha Mohammed Ftouni waliuawa katika shambulio la makusudi la Israeli huko Choueifat, Lebanon, Machi 29, 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *