Jeshi la Iran lilitangaza siku ya Jumamosi kuwa vikosi vyake vimeua au kuwajeruhi zaidi ya wanajeshi 500 wa Marekani katika mashambulizi yaliyolenga maficho mawili ya Marekani huko Dubai.

Tangazo kutoka Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya, kituo kikuu cha kamandi cha majeshi ya Iran, limesema kwamba wanajeshi wa Marekani wamekimbia kambi zao za kawaida za kikanda kufuatia mashambulio yanayoendelea ya Iran na kujikusanya katika maeneo mawili fiche nje ya mji wa Dubai. Kwa mujibu wa Luteni Kanali Ebrahim Zolfaqari, Msemaji wa Jeshi la Iran, maficho mamoja yalihifadhi zaidi ya askari 400 na ya pili zaidi ya askari 100. Maeneo yote mawili yalipigwa na makombora na ndege zisizo na rubani zilizorushwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Kikosi cha Wanaanga na Wanamaji mwishoni mwa Ijumaa.

“Mashambulizi hayo yaliwasababishia hasara kubwa maadui. Magari ya wagonjwa yalikuwa yakisafirisha wanajeshi wa Marekani, wakiwemo makamanda, kwa saa kadhaa kufuatia mashambulizi hayo,” msemaji huyo amesema.

Serikali ya Marekani haijasema lolote kuhusu mashambulizi hayo mapya ya Iran. Ripoti mbalimbali na taarifa za kijeshi zinaonyesha kuwa utawala wa Trump unaficha kwa makusudi idadi halisi ya askari wa Marekani waliouawa na kujeruhiwa. Lengo ni kudumisha kile kinachodaiwa kuwa uungaji mkono wa umma kwa vita vinavyoonekana na wengi kama visivyoungwa mkono zaidi nchini Marekani katika miongo ya hivi karibuni.

Utawala wa Trump unadai ni wanajeshi 14 pekee wa Marekani ndio wameuawa tangu kuanza kwa vita hivyo Februari 28. Hii ni licha ya Iran kuharibu vibaya kambi 17 za Marekani katika nchi saba za Kiarabu, huku ikishambulia pia makazi ya siri ya wanajeshi wa Marekani katika nchi hizo.

Hofu pia inaongezeka nchini Marekani kwamba Trump hivi karibuni anaweza kupanua uchokozi wa nchi hiyo ili kujumuisha askari wa nchi kavu, jambo ambalo wachambuzi wa masuala ya kijeshi wanasema litasababisha maafa makubwa kwa wanajeshi wa Marekani. Baadhi ya wanajeshi waliolengwa na Iran siku ya Ijumaa wanaaminika kuwa walikuwa sehemu ya wanajeshi ambao Marekani inapanga kuwatumia katika uvamizi wa nchi kavu dhidi ya Iran.

Pia mapema Jumamosi, meli ya msaada ya jeshi la Marekani ililengwa na vikosi vya jeshi la Irani ikiwa “umbali mkubwa” katika Bandari ya Salalah nchini Oman, kulingana na taarifa tofauti za Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa Iran inaheshimu mamlaka ya kitaifa ya Oman, ambayo ni “taifa dugu na rafiki.”

Iran pia ilitungua ndege ya kivita ya Marekani aina ya F-16 mapema Jumamosi, na hivyo kufanya idadi ya ndege za kivita za adui ambazo zimelengwa kwa mafanikio katika muda wa wiki nne zilizopita kufikia nane. Kulingana na taarifa ya IRGC, F-16 hiyo lifanikiwa kutua kwa dharura Saudi Arabia baada ya kupigwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *